Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wazinduliwa ili kulinda watetezi wa haki za binadamu

Utafiti wazinduliwa ili kulinda watetezi wa haki za binadamu

Vitisho dhidi ya watetezi wa haki za binadamu vinaongezeka kila uchao, wengine wakiuawa, wakiteswa na hata kukumbmwa na vitisho, amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michel Fort.

Ni kwa mantiki hiyo mtaalamu huyo leo ametangaza uzinduzi wa utafiti utakaofanyika duniani kote kwa lengo la kubainisha mbinu bora ambazo serikali zinazopinga kazi za watetezi hao, zinaweza kutumia ili kuwalinda badala ya kuwashambulia.

Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema madhila dhidi ya watetezi wa haki huchagizwa na serikali na hata vikundi vya kiraia ikiwemo vya kidini, na hivyo utafiti utaonyesha mifano bora ya kuwalinda ili iweze kuigwa na nchi nyingine.

Matokeo ya utafiti huo yatatumika kuchagiza mjadala wakati wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi Machi mwakani.