Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mifumo bora ya hakimiliki ni kichochea cha ubunifu:WIPO

Mifumo bora ya hakimiliki ni kichochea cha ubunifu:WIPO

Mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu umuhimu wa hakimiliki barani Afrika unaendelea huko Dakar, Senegal ukileta pamoja zaidi ya washiriki 400 wakiwemo viongozi wa shirika la hakimiliki duniani WIPO, wanamuziki na waigizaji. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry amesema Afrika ni chimbuko la binadamu na kwa mantiki hiyo ni vyema kuendeleza ubunifu kwenye eneo hilo kwa kuzingatia umetokana na binadamu.

Hata hivyo amesema mifumo na sera bora za hakimiliki ndiyo vinaweza kuchanua ubunifu miongoni mwa raia wa bara hilo na hivyo kuinua ukuaji uchumi katika nchi zao na hata kuendeleza vipaji kwa kuwa wabunifu watanufaika na matunda ya kazi zao.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Elijah Zgambo, mcheza dansi na mjasiriamali kutoka Zambia.

(Sauti ya Elijah)

“Tunaamini kwamba kuna vipaji vingi sana nchini mwetu, hivyo tukiwa na taarifa sahihi na kufahamiana na watu tunaweza kusambaza vipaji hivyo duniani.”