Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuangazia El Niño ya mwaka huu kufanyika Marekani

Mkutano kuangazia El Niño ya mwaka huu kufanyika Marekani

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu El Niño utafanyika nchini Marekani kuanzia tarehe 17 mwezi huu, wakati huu ambapo hali hiyo ya hewa imeanza kutikisa na kuleta madhara katiak baadhi ya maeneo duniani.

Taarifa iliyotolewa leo imesema lengo la mkutano  huo ni kutathmini El Niño  yam waka huu na madhara yanayoweza kutokea, kubaini uhusiano kati yake na mabadiliko ya tabinachi pamoja na kuimarisha mashauriano kati ya wanasayansi wa mazingira na wapanga maendeleo.

Miongoni mwa wazungumzaji kwenye mkutano huo wa siku mbili ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la hali ya hewa duniani, WMO na taasisi ya utafiti wa hali ya hewa duniani.

Tayari El Niño imesababisha ukame na mafuriko katika nchi mbali mbali duniani ikiwemo Ethiopia na Somalia ambapo imeelezwa kuwa dunia imejiandaa kukabiliana nayo lakini madhara ya kiuchumi na kijamii yatokanayo na hali hiyo ya hewa yatasalia kwa muda.

Mara ya mwisho El Niño ilitokea mwaka 1997/98 na kutumbukiza nyongo maendeleo yaliyokuwa yamepatikana.