Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takwimu za makabila ni muhimu katika kupambana na ubaguzi:Ruteere

Takwimu za makabila ni muhimu katika kupambana na ubaguzi:Ruteere

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina za kisasa za ubaguzi Mutuma Ruteere leo ametoa wito kwa serikali ziimarishe ukusanyaji takwimu ili kuweza kupata tathmini sahihi ya makundi yaliyo hatarini zaidi kukumbwa na ubaguzi huo.

Kwenye ripoti yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo, Bwana Ruteere amesema ukosefu wa takwimu za aina hiyo huzuia utungaji wa sera bora na huchochea ukwepaji sheria.

Amesisisitiza umuhimu wa kuwa na takwimu zinazoonyesha kabila la watu katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, huku akitambua wasiwasi wa baadhi ya nchi ambazo zinaogopa kukusanya takiwmu zinazoonyesha makabila.

Bwana Ruteere amewaondoa hofu hiyo akisema cha msingi ni kulinda siri na haki za watu husika akiweka bayana kuwa usawa umeelezwa wazi kwenye lengo namba 17 la maendeleo endelevu linalotaka kila mtu ajumuishwe katika ngazi zote.

Hata hivyo ameongeza kwamba nchi zinapazwa kusaidiwa ili kuimarisha uwezo wao wa kukusanya takwimu za aina hiyo.