Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri usalama wa chakula: Hilal Elver.

Mabadiliko ya hali ya hewa huathiri usalama wa chakula: Hilal Elver.

Mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha matishio ya ukosefu mkubwa wa usalama wa chakula hatua inayoweza kusababisha ongezeko la wagonjwa milioni 600 wa utapiamlo ifikapo mwaka 2080 amesema mtaalamu maalum wa Umoja kuhusu haki ya chakula Hilal Elver.

Amesema kuongezeka kwa joto na kiwango cha bahari, mafuriko na ukame kuna madhara makubwa katika haki ya chakula kwa kufafanua kuwa madhara yake ni katika mazao ,mifugo, uvuvi, na kwa ujumla ustawi wa watu.

Kadhalika Bi Elver ameonya kuwa uzalishaji wa kiwango kikubwa ili kukidhi uhitaji wa soko la chakula sio suluhisho sadhihi katika kilimo.

Amesema kuna haja ya mabadiliko makubwa kutoka kilimo cha viwanda hadi mfumo utakaosaidia mzunguko wa vyakula vya kijamii, kulinda wakulima wadogowadogo kuheshimu haki za binadamu, demokrasia ya chakula na utamaduni huku ulinzi wa mazingira na chakula chenye afya ukizingatiwa.