Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya watoto ya Zanzibar kupata tuzo ni jambo sahihi: UNICEF Tanzania

Sheria ya watoto ya Zanzibar kupata tuzo ni jambo sahihi: UNICEF Tanzania

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini Tanzania, ilikuwa jambo sahihi kabisa kwa sheria mpya ya watoto ya Zanzibar iliyoundwa mwaka 2011 kwa ushirikiano wa UNICEF kupatiwa tuzo ya Future Policies kwani sheria hiyo imeleta mabadiliko makubwa kwenye jamii.

Hayo amesema Ahmed Rashid Ali mtalaam wa masuala ya ulinzi wa mtoto wa UNICEF visiwani Zanzibar alipozungumza na Priscilla Lecomte katika mahojiano maalum baada ya tuzo hiyo kutolewa. Je kwa nini anasema hayo? Basi ungana nao kwenye mahojiano haya ambapo anaanza kwa kuelezea hali ya watoto Zanzibar na sheria yao.