Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia Iraq waendelea kuteseka katika machafuko: UNAMI

Raia Iraq waendelea kuteseka katika machafuko: UNAMI

Takribani watu 700 wameuwawa huku wengine zaidi ya 1,200 wakijeruhiwa mwezi Oktoba kutokana na mashambulizi ya kigaidi, na machafuko hususani yale yanayohusisha silaha umesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI.

Kwa mujibu wa UNAMI katika taarifa inayoangazia vifo na majeruhi kutokana na machafuko nchini humo, idadi hiyo pia inahusisha mamia ya polisi wa kiraia na vikosi pamoja na wanamgambo..

Mwakilishi maaalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Ján Kubiš amesema takwimu hizo zinadhihiridha mateso ambayo watu wa nchi hiyo wanapitia kufuatia machafuko na kuisema kuwa ana matumiani adha hizo zitafikia ukomo wake kutokana na msaada wa umuiya ya kimataifa.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa Baghdad ndiyo mji ulioathiriwa zaidi kutokana na idadi kubwa ya vifo na majeruhi.