Mkuu wa OCHA DRC alaani utekaji wa wahudumu 14 wa kibinadamu
Mratibu wa kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mamadou Diallo, amelaani utekaji wa wahudumu 14 wa kibinadamu wa shirika moja lisilo la kibinadamu la Kongo linalofanya kazi katika eneo la Rutshuru, mkoa wa Kivu Kaskazini.
Akilaani utekaji huo wa Jumapili Novemba pili, Bwana Diallo amesema kitendo hicho kinakwamisha shughuli za kibinadamu na ni ukiukaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.
Aidha, ametoa wito waachiliwe huru mara moja wahudumu hao, akiongeza kuwa utekaji huo unathibitisha mazingira tete yanayoikabili kazi ya mashirika mengi ya kibinadamu, ambayo wahanga wake wa kwanza hua ni wenyeji.