Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa redio laanza mjini Geneva

Mkutano wa kimataifa wa redio laanza mjini Geneva

Mkutano wa kimataifa wa majuma matatu kuhusu mawasiliano ya redio na mikataba husika, umefunguliwa leo mjini Geneva Uswisi ambapo pia mapitio ya kanuni kuhusu redio yatafanyika.

Katika mahojiano na idhaa hii mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Balozi Modest Mero amesema ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano suala la masafa ya redio na changamoto zake limejadiiwa.

Amesema barani Afrika changamoto katika hilo ni.

(SAUTI BALOZI MERO)

Zaidi ya washiriki Elfu Tatu kutoka nchi 160 kati ya 193 wanachama wa shirika la mawasiliano duniani, ITU wanashiriki mkutano huo.