Maelfu wazidi kuvuka Mediteranea kwenda Ulaya kusaka hifadhi:UNHCR

Maelfu wazidi kuvuka Mediteranea kwenda Ulaya kusaka hifadhi:UNHCR

Janga la wahamiaji na wakimbizi wanaovuka bahari ya Mediteranea kwenda Ulaya kusaka hifadhi limezidi kushika kasi ambapo mwezi uliopita pekee idadi yao imefikia watu 218, 000. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema idadi hiyo ni kubwa na inakaribia watu waliovuka bahari hiyo kipindi chote cha mwaka jana.

Takwimu za hivi punde zaidi zinasema Ugiriki inaendelea kuwa lango la kuingilia kwa idadi kubwa ya wakimbizi hao ikifuatiwa na Italia, licha ya mazingira magumu ya hali ya hewa baharini.

Mwaka huu pekee zaidi ya watu Laki Saba wamefanya safari hiyo ya hatari wengi wakitokea Uturuki na nusu yao ni raia wa Syria ambapo mtu mmoja kati ya wanne ni mwanamke au mtoto.

Wengine wanatoa Afghanistani, Iraq na Eritrea ambapo UNHCR imesema katika safari hiyo ya kuvuka bahari ya mediteranea zaidi ya watu 3,400 wamefariki dunia mwaka huu pekee.

.