Baraza la Usalama lalaani shambulizi la kigaidi Mogadishu, Somalia

1 Novemba 2015

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali shambulizi lililotekelezwa leo Novemba mosi na Al-Shabaab dhidi ya hoteli ya Sahafi mjini Mogadishu, Somalia, ambalo lilisababisha vifo na majeraha kadhaa.

Wajumbe hao wa Baraza la Usalama wameeleza huzuni na rambirambi zao kwa familia za wahanga, pamoja na kwa watu na serikali ya Somalia, huku wakiwatakia upanaji haraka majeruhi.

Aidha, wajumbeo hao wamepongeza hatua za haraka zilizochukuliwa na jeshi la kitaifa la Somalia katika kujibu shambulizi hilo.

Wamekariri pia kuwa ugaidi wa aina zote ni moja ya tishio kubwa zaidi kwa amani na usalama duniani, na kwamba vitendo vyovyote vya kigaidi haviwezi kukubalika, bila kujali vinachochewa na nini, wapi na nani anayevifanya.

Aidha, wamekariri pia haja ya kuwafikisha wahalifu, wapangaji na wafadhili wa vitendo hivyo haini vya kigaidi mbele ya sheria, na kutoa wito kwa serikali zote zishirikiane na serikali ya Somalia katika kutekeleza hili, kulingana na wajibu wao chini ya sheria ya klimataifa na maazimio husika ya Baraza la Usalama.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter