Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO, HRCI na IJS zataka ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari ukomeshwe Iraq

UNESCO, HRCI na IJS zataka ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari ukomeshwe Iraq

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Kamishna wa Haki za Binadamu Iraq, HRCI, na Shirika la Wanahabari Iraq, IJS, yametoa wito kwa mamlaka za Iraq zichukue hatua zote zipasazo kuhakikisha kuwa uchunguzi unafanyika na mashtaka kufunguliwa kwa uhalifu wote unaotendwa dhidi ya wanahabari nchini Iraq.

Katika taarifa ya pamoja kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya kumaliza ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari hapo kesho Novemba 2, Mwakilishi wa UNESCO Iraq, Axel Plathe, Kamishna wa Haki za Binadamu Iraq, Athmar al Shatry na Rais wa IJS, Moaid Al-Lami, wamesema mamlaka za Iraq zinapaswa kutunga sheria, kuongeza uwezo na kuelekeza rasilmali katika kuwezesha kukabiliana na ukwepaji sheria kwa wanaotenda uhalifu dhidi ya wanahabari. Wamesema ukwepaji sheria kwa uhalifu dhidi ya wanahabari unakwenda kinyume na kila kitu wanachokishabikia, maadili na dhamira ya pamoja.

Usalama wa wanahabari nchini Iraq ni mbaya mno, kukiwa na idadi kubwa ya mashambulizi dhidi ya wanahabari na kuendelea kukwepa sheria kwa wanaotenda mashambulizi hayo. Zaidi ya visa 100 vya mauaji ya wanahabari havijachunguzwa vyema kufikia sasa.