Ban ahuzunishwa na ajali ya ndege ya Urusi

Ban ahuzunishwa na ajali ya ndege ya Urusi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameelezwa kuhuzunishwa mno na habari za ajali ya ndege ya Urusi katika rasi ya Sinai nchini Misri, ambapo abiria wote 224 na wafanyakazi wa ndege hiyo walifariki dunia.

Ndege hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Sharm el-Sheikh kwenda St Petersburg wakati wa ajali hiyo.

Taarifa ya msemaji wake imesema kuwa Katibu Mkuu ametuma rambirambi zake kwa familia za wahanga, pamoja na kwa watu na serikali ya Urusi.