Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

uhifadhi wa sauti na video Afrika Mashariki

uhifadhi wa sauti na video Afrika Mashariki

Oktoba 27 ni siku ya kimataifa ya uhifadhi wa sauti na video.Siku hii ambayo ilipitishwa mwaka 2005 na BAraza Kuu la Umoja wa Mataifa inalenga kuchagiza uelewa wa hatua madhubuti za utunzaji wa nyaraka za sauti na video kama kiungo muhimu cha utambulisho wa kitaifa.

Katika ujumbe wa mwaka huu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, Irina Bokova amesema kwamba kuna miaka 10 hadi 15 ya kubadilisha sauti za video zilizopo kutoka analojia kwenda dijitali ili kuhakikisha uhifadhi wake.

Bi Bokova ameongeza kwamba ni muhimu kwamba historia hii ieleweke na isambazwe si tu kwa ajili ya utambulisho lakini kwa ajili ya kufanikisha uelewa zaidi wa uhusiano na changamoto za jamii.

Vipindi vya radio, televisheni na filamu ni moja ya urithi wa  karne ya 20 na 21 kwani vinasaidia katika kuhifadhi utamaduni wa watu. Kulingana na UNESCO urithi wa sauti na video u hatarini na ndipo sasa kuna haja ya kuhakikisha uhifadhi wake. Je ni mikakati ipi ambayo imewekwa kuhakikisha hili linafanikishwa Afrika Mashariki? Tuanzie nchini Uganda ambapo John Kibego amevinjari katika kituo kimoja cha televisheni kujionea uhifadhi wa sauti na video.

(SAUTI KIBEGO)