Skip to main content

Kenya yapazia sauti muundo wa Baraza la Usalama la UM

Kenya yapazia sauti muundo wa Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa chombo cha kusimamia amani na usalama, linakosa muundo ambao unakwenda na uhalisia wa ulimwengu wa sasa katika kutekeleza majukumu yake.

Amesema Balozi Anthony Andanje, kutoka Idara ya masuala ya ushirikiano ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya wakati akihutubia kikao cha wazi cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, kuhusu hoja ya uwakilishi wenye uwiano sawa kwenye Baraza la Usalama la Umoja huo.

Balozi Andanje amesema..

(Sauti ya Balozi Andanje)

 “Afrika, ambayo ndiyo ina ajenda kubwa zaidi katika baraza la usalama na ni kitovu cha kazi kubwa ya chombo hicho, haina sauti kwenye Baraza hilo. Hii siyo tu ni ubaguzi bali pia si  haki na sawa. Ujumbe wangu unashawishika kuwa ni vyema Baraza liwe na uwezo wa kukidhi viwango na matakwa ya karne ya 21. Linapaswa kupata uhalali kwa kuzingatia uwajibika na demokrasia katika taratibu zake za kuchukua uamuzi na uwakilishi.”