Idadi ya vifo vya wahamiaji mwaka huu yafikia 3, 329: IOM

30 Oktoba 2015

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limesema idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliokufa maji kutokana na boti zao kuzama bahari ya Mediteranea  imefikia 3.329 mwaka huu pekee.

Shirika hilo limetoa takwimu hizo likizingatia pia tukio la jana na juzi la vifo vya wahamiaji wengine wanne huko Hispania likisema idadi hiyo ni kubwa kulinganishwa na watu 3279 mwaka jana pekee.

Kelly Namia, afisa wa IOM huko Ugikriki ambaye alikuwepo wakati mojawapo ya boti ikizama hapo jana amesema janga katika bahari hiyo halina mwisho.

Wakati wa janga hilo watu wanaokisiwa kuwa 14 walipoteza maisha yao, huku wahamiaji wengine 138 wakiokolewa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter