Skip to main content

Mwimbaji wa Ghana MzVee atumia muziki katika vita dhidi ya umaskini

Mwimbaji wa Ghana MzVee atumia muziki katika vita dhidi ya umaskini

Katika mflulizo wa Makala kuhusu matumizi ya muziki kuhamasisha maendeleo, tunakutana na nyota wa Ghana, MzVee.

MzVee ambaye ameanzisha mfuko wa kuwasaidia wasichana kupata elimu, ni maarufu sana kwa wimbo, Natural Girl, ambao anautumia kutoa wito kwa wasichana kuchagua mustakhbali wao na kufuata ndoto zao.

Aidha, MzVee amekuwa akitumia muziki kuchagiza watu wajikite katika shughuli za kuleta maendeleo, zikiwemo elimu na kupigana na umaskini. Kwa mengi zaidi, ungana na Joshua Mmali katika Makala ifuatayo.