Surua yatikisa jimbo la Katanga, DRC, watu 500 wafariki dunia

30 Oktoba 2015

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, jimbo la Katanga linakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa ugonjwa wa Surua kuwahi kukumba eneo hilo katika miaka ya karibuni.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu, OCHA imesema hadi sasa watu takribani 500 wamefariki dunia tangu kuanza kwa mwaka huu na wengi wao ni watoto walio na umri wa chini ya miaka Mitano.

Idadi hiyo ya vifo ni kati ya wagonjwa 3,500 walioripotiwa, idadi ambayo ni kubwa kulinganisha na visa vya Surua kwenye jimbo hilo katika miaka mitatu iliyopita.

Kwa sasa OCHA imesema katika taarifa yake kuwa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la afya, WHO na lile la kuhudumia watoto, UNICEF yanashirikiana kutokomeza ugonjwa huo kupitia nji mbali mbali ikiwemo kutoa chanjo, na kusaidia vituo vya afya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter