Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miji endelevu ni chombo cha maendeleo katika Ajenda 2030 ya SDGs- UN-Habitat

Miji endelevu ni chombo cha maendeleo katika Ajenda 2030 ya SDGs- UN-Habitat

Kuelekea Siku ya Miji Duniani hapo kesho Oktoba 31, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Makazi katika Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, Joan Clos, amesema kubuni mpangilio wa miji ni suala muhimu katika kuifanya miji iwe endelevu. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Bwana Clos amesema katika kutunga ajenda ya maendeleo endelevu iliyopitishwa mwezi uliopita, ilitambuliwa kuwa miji ni chombo cha maendeleo na cha maendeleo endelevu.

Ameinukuu kauli ya Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuwa, ufanisi wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu, SDGs, itategemea maendeleo na uendelevu wa miji. Kwa mantiki hiyo, amesisitiza kilicho muhimu katika kutunga mpangilio na umbo la mji

Tunapobuni mji, ubora wa mtungo ni muhimu katika kubuni maeneo ya umma yaliyo rafiki kwa kila mtu, na inayowezesha ubora wa maisha wanayohitaji watu. Ujenzi wa miji ni kuchanganya vyema maeneo ya umma na maeneo ya majengo ya watu binafsi.”