Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shehena ya UNMISS haikuwa ya silaha

Shehena ya UNMISS haikuwa ya silaha

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudani Kusini Ellen Margrethe Loej amesema msafara wa walinda amani uliotekwa nyara mapema wiki hii na waasi wa kikundi cha SPLM/A-Upinzani huko jimbo la Upper Nile haukuwa unasafirisha aina  yoyote ya silaha.

Katika taarifa yake iliyosomwa na msemaji wake, Ariane Quentier, Bi. Loej ambaye pia ni mkuu wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS amesema..

(Sauti ya Arian)

Nakanusha kwa dhati taarifa zozote za vyombo vya habari kuwa boti husika ilikuwa inasafirisha shehena ya silaha za aina yoyote na nasisitiza kuwa shehena yote ya mafuta ililenga kuwafikia kituo cha UNMISS kilichoko Renk na si kwa ajili ya matumizi ya wapinzani.”

Kufuatia mashauriano kati ya SPLM/A upinzani na UNMISS, tayari walinda amani 18 lakini bado wakandarasi 12 wa UNMISS ambao ni raia wa Sudan Kusini wanashikiliwa ambapo Bi. Loej amesihi waachiliwe huru mara moja kwani mashambulizi dhidi yao ni shambulizi dhidi ya Umoja wa Mataifa.