Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 60 baada ya kujiunga na UM, mchango wa Hispania wamulikiwa

Miaka 60 baada ya kujiunga na UM, mchango wa Hispania wamulikiwa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amelipongeza taifa la Uhispania kwa mchango wake mkubwa kwa Umoja wa Mataifa, leo ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka 60 tangu nchi hiyo ijiunge na Umoja huo.

Akizungumza  leo wakati wa maadhimisho hayo mjini Madrid, Hispania, Bwana Ban amemulika mchango wa nchi hiyo katika kupambana na ugaidi, kulinda amani duniani, kuunda na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, na kuangazia suala la wanawake vitani.

Ban kwenye hotuba  yake ametoa pia wito Hispania iwe na uongozi zaidi unaoustahili kwenye jukwaa la kimatiafa, ili kusaidia kukuza mustakabali bora kwa wote.

Punde baada ya mkutano huo, Bwana Ban amekutana na mfalme Felipe wa VI ambapo wamezungumza kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na umuhimu wa kuafikiana kuhusu mabadiliko ya tabianchi, mjini Paris, mwisho wa mwaka huu.