Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkindu hatarini kutoweka Uganda

Mkindu hatarini kutoweka Uganda

Nchini Uganda, mkindu ni mti ambao umekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi. Hata hivyo kutokana na uingiliaji wa maeneo oevu na ukataji holela wa miti nchini humo, eneo la magharibi mwa nchi ambalo lina idadi kubwa ya miti hiyo kuna hatari kuwa itatoweka na hivyo kutumbukiza nyongo ustawi wa wananchi. Je mkindu una manufaa gani na ni hatua gani zinazochukuliwa kuulinda dhidi ya uchafuzi?. John Kibego anakujuza katika makala ifuatayo.