Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawa ya kuongeza nguvu michezoni yapingwa Paris

Madawa ya kuongeza nguvu michezoni yapingwa Paris

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO linaendesha mkutano wa siku mbili mjini Paris Ufaransa kuhusu mkataba wa kupinga matumizi ya madawa  kuongeza nguvu katika michezo. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Mkutano huo wa tano wa nchi wanachama zilizosaini mkataba huo umeanza leo ambapo UNESCO inaadhimisha muongo mmoja wa kupambana na matumizi ya madawa katika michezo katika nchi 182.

UNESCO inazingatia kuwa kuwaelimisha vijana wanawake na wanaume kuhusu hatari ya matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu ni muhimu katika kuondoa janga hilo kwa kizazi kijacho cha wanariadha.

Wawakilishi zaidi ya 250 wa mataifa tofauti na wale wa jumuiya za michezo na wanamichezo wanatarajiwa kushiriki ili kujaidili changamoto za kukabiliana na matumizi ya madawa hayo na kupendekeza suluhisho wakati huu ambapo suala la matumizi ya madawa ili kuboresha mafanikio husuani kwa vijana barubaru na vijana pamoja na wanariadha wa ridhaa likikua.

Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mikutano hiyo, UNESCO itawakaribisha washindi wa medali za Olimpiki kama vile Becki Scott kutoka Canada.