Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Libya kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabomu yaliyotegwa ardhi.

Vijana Libya kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabomu yaliyotegwa ardhi.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umekamilisha mafunzo kwa vijana 16 watakaohamasisha jami kuhusu hatari za mabomu ya kutegwa ardhini.

Vijana hao kutoka kusini mwa nchi hiyo walipata mafunzo hayo ya wiki mbili  nchini Tunisia kwa lengo la kupunguza ajali zitokanazo na mabomu hayo, hasa miongoni mwa watu waliolazimika kuhama makwao kutokana na machafuko.

Wahamasishaji hao wanatakiwa kuwa wameelimisha watu wapatao 5,600 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na watatumia mbinu mbali mbali ikiwemo michezo na maigizo.