Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawe yaliyokuwa janga sasa yaleta nuru huko Goma

Mawe yaliyokuwa janga sasa yaleta nuru huko Goma

Mradi wa benki ya dunia unoatekelezwa huko jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, umeanza kuleta matumaini kwa wakazi wa mji wa Goma ambao mlipuko wa volkano ulikata mawasiliano ya safari za anga na kusambaratisha maisha yao.

Mlipuko huo wa mwaka 2002 uliharibu uwanja wa ndege wa Goma na kusababisha maeneo mengi kufunikwa na mawe makubwa ambayo hata hivyo kwa sasa yamegeuka njia ya wanawake kujipatia kipato kwa kuyavunja ya kupata kokoto.

Louise Bahati, ni mmoja wa wanawake waliokusanyika na kuunda kikundi cha kujikwamua kupata kipato.

(Sauti ya Louise)

Mradi huo wa benki ya dunia pamoja na kuimarisha uwanja wa ndege wa Goma ili kuweza kuanza upya safari za kimataifa, unalenga kuweka mbinu za kubaini uwezekano wa mlipuko wa volkano na hivyo kupunguza athari.