Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu bilioni tatu waathiriwa na melengelenge ya neva ngozini: WHO

Watu bilioni tatu waathiriwa na melengelenge ya neva ngozini: WHO

Zaidi ya watu bilioni 3.7 duniani wenye umri wa chini ya miaka 50 sawa na asilimia 67 ya wakazi wote duniani, wameathiriwa na virusi aina ya kwanza vya ugonjwa wa melengelenge ya neva ngozini

limesema shirika la afya ulimwenguni WHO. Taarifa ya Joseph Msami inafafanua zaidi.

(TAARIFA YA MSAMI)

Kwa mujibu wa tathimini ya kwanza ya WHO iliyochapishwa leo, ugonjwa huo ambao huenezwa na virusi aina ya kwanza HSV-1 na ya pili HSV-2 , imeeleza kuwa kirusi cha kwanza huenea kupitia migusano ya kimwili  hususani kupitia midomo.

WHO inasema kuwa kirusi cha kwanza ndiyo hueneza malengelenge ya neva katika viungo vya uzazi na kwamba watu takribani milioni 140 walioko kati aya umri wa miaka 15-49 wameathiriwa na HSV-1

Dk Marleen Temmerman, ni mkuu wa idara ya afya ya uzazi na utafiti ya WHO

( SAUTI DK MARLEEN)

‘‘Kwa hakika tunahitaji kuongeza kasi ya hatua za chanjo dhidi ya virusi vya ugonjwa huu kwani utafiti unaonyesha kuwa ikiwa chanjo imeandaliwa kuzuia maambukizo ya kirusi HSV-2, pia huzuia HSV-1 na hivyo itakuwa na manufaa zaidi.’’