Baraza la Usalama lasikia ripoti kuhusu Darfur na ujumbe wa UNAMID

28 Oktoba 2015

Suluhu la kina kwa mzozo wa Darfur litakaloruhusu kurejea nyumbani kwa zaidi ya watu milioni 2.6 waliofurushwa makwao, linahitaji kwanza mapatano ya kisiasa baina ya serikali na vikundi vilivyojihami, amesema Naibu Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani, Edmond Mullet. Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Bwana Mamesema hayo akilihutubia Baraza la Usalama, ambalo limekutana leo kuhusu ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID.

Kuhusu mzozo wa Darfur, Bwana Mullet amesema nia ya pande kinzani kufanya mazungumzo kuhusu kumaliza uhasama pamoja na mashauriano ya kitaifa jijini Addis Ababa ni hatua ya kupongezwa katika kutimiza lengo la kufikia suluhu la kina kwa mzozo huo.

Aidha, Mullet amezungumza kuhusu changamoto zinazoukumba ujumbe wa UNAMID, wakati ukitekeleza majukumu ya mamlaka yake, na kutoa wito kwa serikali ya Sudan iondoe vikwazo vinavyotatiza kazi ya ujumbe huo.

Sauti ya Mulet

Ningependa kutoa wito pia kwa serikali iondoe vikwazo vyote kwa usafiri huru wa wafanyakazi na vyombo vya UNAMID, hususan kuhusu kufikia maeneo yenye machafuko na muhimu zaid, utoaji wa visa, kama inavyotakiwa katika makubaliano kuhusu hadhi ya vikosi vya UNAMID.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter