Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko baina ya Waisrael and Wapalestina yataleta janga yasipokomeshwa- Zeid

Machafuko baina ya Waisrael and Wapalestina yataleta janga yasipokomeshwa- Zeid

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein, ameonya kuwa machafuko baina ya Waisraeli na Wapalestina yanaweza kusababisha janga kubwa iwapo hayatakomeshwa.

Akihutubia Baraza la Haki za Binadamu wakati wa ziara ya Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, Kamishna Zeid amesema wimbi la machafuko hivi karibuni limesababisha vifo vya Wapalestina 58 na kuwajeruhi 2,100, huku Waisraeli 11 wakiuawa na 127 kujeruhiwa.

Ameongeza kuwa machafuko hayawezi kuwa suluhu kwa malalamishi, hata yawe ya aina gani.

Mzozo huu ni hatari sana kwa sababu unatokana na uoga, kwani watu kutoka pande zote wanaishi kwa kuogopana na hata kuhofia mustkakhabali wao. Kuna uwezekano kuwa iwapo machafuko haya yataendelea kwa misingi ya dini, utatusongesha karibu na mgogoro mkubwa zaidi. Ukanda huo wenye maafa tayari hauhitaji hili.”