Maisha ya watoto hatarini Afghanistan na Pakistan baada ya tetemeko la ardhi

Maisha ya watoto hatarini Afghanistan na Pakistan baada ya tetemeko la ardhi

Maisha ya watoto waliojeruhiwa na tetemeko la ardhi lililokumba maeneo ya milima ya Afghanistan na Pakistan jumatatu hii yako hatarini kwa sababu hawafikiwi ili kupatiwa misaada, amesema leo Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ukanda wa Asia Kusini, Karin Hulshof.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNICEF imesema kwamba nusu ya watu 1,000 waliojeruhiwa ni watoto. Aidha, miongoni mwa watu 200 waliouawa, 12 walikuwa ni wanafunzi wa kike.

UNICEF imeeleza kwamba maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi hayafikiki kwa sababu ya mvua na theluji vinazidi kuanguka na kunyesha, mawasialiano kukatika na barabara kufungwa.

Amesema mazingira hayo magumu na baridi vinahatarisha maisha ya maelfu ya familia zilizokumbwa na tetemeko hilo.

UNICEF Afghanistan na Pakistan inasiadia jitihada za serikali katika kusambaza usaidizi wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu.