Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Australia na Nauru watolewa wito kumsaidia mwanamke aliyedaiwa kubakwa

Australia na Nauru watolewa wito kumsaidia mwanamke aliyedaiwa kubakwa

Australia na taifa la Pasifiki la Nauru wametolewa wito kumsaidia mwanamke wa Somalia ambaye anadaiwa kubakwa huko Nauru, huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake tete ya kiakili na kimwili.

Taarifa kamili na Abdullahi Boru

(Abdullahi Taarifa)

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR, imesema kuwa mwanamke huyo ambaye amepewa jina "Abyan”  ili kumlinda asitambuliwe, ana mimba ya wiki 15 na ametatizika kiakili kufuatia madhila aliyokumbana nayo.

Ofisi ya OHCHR imesema inafahamu kuongezeka kwa madai ya ubakaji tangu Australia ilipoanza sera mpya ya kuhamishia watu wanaotafuta hifadhi taifa la kisiwa  cha Nauru kwa ajili ya usajili mwaka 2012.

Rupert Colvile ni msemajia wa OHCHR

(Sauti colvile )

Yuko katika hali dhaifu kiakili na kimwili sawa na kupata kiwewe na alichopitia kuanzia siku aliyodaiwa kubakwa... amekataa kutoa taarifa kwa polisi ya Nauru kuhusu mtu aliyembaka kwa sababu ya hofu ya ulipizaji wa kisasi."

Taifa la Nauru lina wasaka hifadhi na wakimbizi 1100 na wakaaji 10,000, na ni karibu Kilomita 3,000 kutoka pwani ya kaskazini ya Australia.