Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wazidi kumiminika Yemen licha ya machafuko

Wahamiaji wazidi kumiminika Yemen licha ya machafuko

Licha ya vita na mzozo wa kibinadamu unaoendelea nchini Yemen, wakimbizi na wahamiaji 70,000 kutoka Ethiopia na somalia wamewasili nchini humo kwa boti tangu mwanzo wa mwaka huu.

Nusu yao wamewasili baada ya mzozo kuanza nchini Yemen mwezi Machi.

Adrian Edwards ambaye ni msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR, ameeleza hay oleo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, akisema safari ya kuvuka bahari ya Arabia ni hatari sana, watu angalau 88 wakiwa wamefariki dunia tangu mwanzo wa mwaka.

Hata hivyo amesema..

(Sauti ya Edwards)

" Wakati huo huo Yemen inaendelea kushuhudia ongezeko la idadi ya watu waliolazimika kuhama makwao. UNHCR imetoa usaidizi wa dharura kwa familia zilizolazimika kukimbia makwao. Kufikia watu walioathirika bado changamoto ya msingi. Wengi wanaohitaji msaada wako kwenye maeneo yasiyofikika. Kinachosikitisha ni kwamba mapigano yanaendelea nchini humo na raia ndio wanateseka."

Kwa mujibu wa UNHCR, idadi ya wakimbizi nchini Yemen inakaribia kufika 265,000, ambapo 250,000 miongoni mwao ni wasomali,