Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lapitisha azimio la kutaka vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba viondolewe

Baraza Kuu lapitisha azimio la kutaka vikwazo vya Marekani dhidi ya Cuba viondolewe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mkutano wa wazi kuhusu umuhimu wa kuondoa vikwazo vya kiuchumi, kibiashara na kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Cuba zaidi ya miongo mitano iliyopita. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Zaidi ya nchi 16 na vikundi nane vya kikanda vilitoa hotuba ambazo pamoja na kukaribisha kurejeshwa kwa uhusiano kati ya Cuba na Marekani zimetaka vikwazo hivyo viondolewe kwa kuwa vinazidi kuleta madhila kwa wananchi wa Cuba.

Nchi zisizofungana na upande wowote zimesema vikwazo vinakwamisha Cuba kushiriki biashara za kimataifa na hata kupata misaada ya kiteknolojia na uwekezaji.

Nalo Kundi la nchi 77 na China kupitia mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa Kingsley Mamabolo likasema..

(Sauti ya Mamabolo)

Mwishoni mwa mkutano  huo wa wazi, Baraza Kuu limepitisha azimio lenye lengo la kusaka kuondolewa kwa vikwazo hivyo ambapo nchi 191 zimeunga mkono ilhali Marekani na Israel zikipiga kura ya hapana.

Upitishwaji wa azimio hilo la leo umekuwa na kura tatu zaidi ikilinganishwa na azimio la awali la mwaka jana.