Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchaguzi Cote d’Ivoire wafanyika kwa amani

Uchaguzi Cote d’Ivoire wafanyika kwa amani

Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa rais nchini Cote d’Ivoire imefanyika jana tarehe 25 Oktoba kwa amani na utulivu.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Hii ni kwa mujibu wa mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI, Aichatou Mindaoudou ambaye ameiambia redio ya Umoja wa Mataifa kwamba hakukuwa na tukio lolote la vurugu nchini humo.

Aidha Bi Mindaoudou ameeleza kwamba Umoja wa Mataifa umesaidia tume huru ya uchaguzi katika maandalizi ya uchaguzi na ulinzi wa usalama kupitia polisi 6,000 wa UNOCI. Hata hivyo, ameongeza kwamba UNOCI haishiriki katika hesabu za kura.

Hatimaye Bi Mindaoudou ametuma ujumbe kwa raia wa Cote d’Ivoire, wakati ambapo awamu ya pili inatarajiwa kufanyika tarehe 2, Novemba.

(Sauti ya Bi Mindaoudou)

“Nataka kupongeza raia wa Cote d’Ivoire kwa sababu wameweza kuweka mbele manufaa ya umma na kuheshimu masharti ya demokrasia. Natumai kwamba itaendelea hivyo wakati ambapo tunatarijia kupokea matokeo ya uchaguzi leo au kesho.”