Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Miaka 70 ya Umoja wa Mataifa

Leo tarehe 24 Oktoba ni miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa huko San Francisco nchini Marekani.

Siku hiyo mataifa 50 yalitia saini makubaliano ya kuanzisha chombo hicho kilichokuwa na lengo na kulinda Amani na usalama, kuendeleza ushirikiano baina ya mataifa kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kijamii na kulinda haki za binadamu.

Akizungumza usiku wa Ijumaa kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani wakati wa tamasha maalum la muziki mahsusi kwa siku ya Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema..

(Sauti ya Ban)

"Ushirika wetu unaweza usikose dosari, lakini bila Umoja wa Mataifa nakueleza kuwa dunia yetu ingalikuwa na giza zaidi. Na sasa kwa kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu yanayochochea ustawi, Umoja wa Mataifa umeonyesha njia ya kuwa na maendeleo ya binadamu.”

Kilele cha maadhimisho hayo kilishuhudiwa kuangaziwa kwa rangi ya buluu, rangi rasmi ya umoja wa mataifa kwa majengo na minara 300 maarufu kutoka nchi 75 duniani, likiwewemo jengo la makao makuu ya Umoja huo jijini New York.

Maeneo mengine yaliyoshiriki kuangazia mwanga wa buluu ni pamoja nay ale yaliyoko bara la Australia, Asia, Afrika , Ulaya na Amerika.