Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatujaona nakala ya barua ya UKAWA kwa Umoja wa Mataifa: Alvaro

Hatujaona nakala ya barua ya UKAWA kwa Umoja wa Mataifa: Alvaro

Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez amesema hawajapokea nakala ya barua inayodaiwa kuandikwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini humo inayodaiwa kupinga kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kutaka wananchi kurejea nyumbani punde tu wakishapiga kura.

Akihojiwa na Idhaa hii, Bwana Alvaro amesema..

(Sauti ya Alvaro-1)

Tuna taarifa za barua hiyo lakini ni kwamba hatujapata nakala. Suala hili linavutia sana kwa kuwa kwa mujibu wa sheria hauruhusiwi kuwa ndani ya mita mia mbili za kituo cha kupiga kura. Kesi hiyo imewasilishwa mahakamani na ninaelewa kuwa uamuzi utatolewa haraka. Lakini ni muhimu kufahamu kuwa sheria ya nchi imeweka hilo bayana na sisi kama Umoja wa Mataifa tutaheshimu sheria za nchi.”

Kuhusu mwelekeo wa uchaguzi Bwana Alvaro amesema kampeni zimekuwa za amani na matarajio yao ni kwamba..

(Sauti ya Alvaro-2)

Tunatumai siku ya uchaguzi ambayo ni tarehe 25 Oktoba na hususan mchakato wa matokeo utakaofuatia siku chache, nao utakuwa wa amani. Tunafahamu kuwa bila kujali nani atakayeshinda, mshindi atakuwa kiongozi wa watanzania wote. Halikadhalika watakaoshindwa watakubali kuwa ndio utashi wa wananchi na hivyo wanatakiwa kusonga mbele kuendelea kujenga jamii ya kidemokrasia ya kitanzania.”

Uchaguzi wa Jumapili ni wa rais, wabunge na madiwani ambapo kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi jumla ya watu 23,253,982 wamejiandikisha kupiga kura Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Uchaguzi wa Jumapili ni wa rais, wabunge na madiwani ambapo kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi jumla ya watu 23,253,982 wamejiandikisha kupiga kura Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.