Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tumechukua hatua dhidi ya mlipuko wa kipindupindu: Tanzania

Tumechukua hatua dhidi ya mlipuko wa kipindupindu: Tanzania

Wakati Shirika la afya duniani, WHO likionya juu ya uwezekano wa kuongezeka kwa mlipuko wa Kipindupindu nchini Tanzania wakati huu ambapo utabiri wa hali ya hewa unaashiria mvua kubwa za El Nino, nchi hiyo imefafanua kuwa imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko huo.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania, Dkt. Janeth Mghamba amesema hatua za kudhibiti kuenea zaidi hasa katika maji safi na huduma za kujisafi zimechukuliwa.

(SAUTI DK JANETH)

Dk Janeth pia amezungumzia hatua nyingine zilizochukuliwa kwa kuwashierikisha wadau mbalimabli katika  kudhibiti mlipuko wa kipindupindu.

(SAUTI JANETH)

WHO imesema mji wa Dar es salaam unaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa ambao ni 3,500 tangu mwezi Agosti na kati yao 74 wamefariki dunia.