Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyota wa filamu washiriki kampeni ya kutokomeza utumwa wa kisasa

Nyota wa filamu washiriki kampeni ya kutokomeza utumwa wa kisasa

Wachezaji filamu Robin Wright, David Oyelowo na Balozi mwema wa Shirika la Kazi Duniani ILO, Wagner Moura wameshiriki kwenye kampeni mpya ya ILO kuhusu utumikishwaji wa kisasa, iitwayo Hamsini kwa ajili ya uhuru.

Lengo la kampeni ni kuelimisha jamii ili ishawishi serikali za nchi angalau hamsini kuridhia itifaki ya kupinga aina mpya za utumikishwaji ifikapo mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa ya ILO, Niger ndio nchi ya pekee duniani ambayo tayari imeridhia itifaki hiyo ambayo ina nguvu kisheria.

Wasanii hao wamezindua video ambako wanasimulia hadithi za watu miongoni mwa milioni 21 wanaoathirika na aina mpya za utumwa.