Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoweka bila hiari, hebu tuache kujifanya ni suala la zamani; Wataalamu

Kutoweka bila hiari, hebu tuache kujifanya ni suala la zamani; Wataalamu

Kikosi kazi kuhusu suala la watu kulazimishwa kutoweka bila hiari kimetoa wito kwa nchi kupatia kipaumbele ajenda kuhusu suala hilo.

Kikosi hicho pia, kimetoa wito kwa serikali kushughulikia mabadiliko ya ukiukaji huo wa haki za binadamu na mwelekeo mpya wa watu kulazimishwa kutoweka, kuongezeka kwa shughuli za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na aina mpya ya waathirika.

Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati teule kuhusu kutoweka bila hiari, ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa, jamii haiwezi kufumbia macho sulaa hilo ikidai kuwa ni la zamani, badala yake, msiba unaotokea baada ya mtu kutoweka bila hiari ni lazima utambuliwe kama suala la kisasa ili kuendeleza hatua madhubuti na ya kina kwa ajili ya kutokomeza.

Aidha, wataalamu hao wa haki za binadamu wamesema tangu mwanzo wa mwaka huu, wamekuwa wakishughulikia zaidi ya matukio 150 ya hivi karibuni ya watu kutoweka kote duniani.