Ujasiri wa wanawake ndiyo hunipa ujasiri: Dk Mukwege
Jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza kumeonyeshwa filamu iitwayo mwanaume anayerekebisha wanawake ikiwa inamulika maisha ya Dk Denis Mukwege anayesaidia maelfu ya wanawake waliothiriwa kutokana na ubakaji nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo DRC.
Dk Mukwege ambaye ni mshindi wa tuzo ya Sakharov kutoka Muungano wa Ulaya anayetoa tiba katika mazingira magumu ya machafuko katika hospitlai iitwayo Panzi iliyoko Bukavu DRC, ameiambia idhaa hii muda mfupi baada ya filamu hiyo kile kinachompa hamasa kuendelea na kazi hiyo ngumu.
(SAUTI DK MUKWEGE)
Mahojiano kamili na Dk Mukwege pamoja na undani wa filamu hiyo yatakujia katika matangazo yetu yajayo.