Tanzania imeendelea kuwa na mchango mkubwa kwa Umoja wa Mataifa:UM
Ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa ulioanza hata kabla ya uhuru wa nchi hiyo umezidi kuimarika na taifa hilo limekuwa na mchango mkubwa wa chombo hicho.
Amesema Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez alipohojiwa na Idhaa hii kuhusu maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Bwana Rodriguez amesema hata baada ya uhuru Tanzania imenufaika na miradi ya kiuchumi, kijamii huku yenyewe ikichangia katika shughuli za ulinzi wa amani na kuhifadhi wakimbizi waliokimbia makwao. Kwa hiyo amesema kuendelea mbele..
(Sauti ya Alvaro)
“Kuwa na uongozi thabiti wa serikali kutekeleza miradi ya kipaumbele ya malengo ya maendeleo endelevu. Hiki kitakuwa kipindi muhimu zaidi kwa Tanzania. Tanzania imekuwa na ukuaji mkubwa wa kiuchumi miaka 15 iliyopita. Lakini sasa kuna wito wa dhati wa kuondokana na umaskini kwa juhudi zaidi.”