Skip to main content

Mamilioni ya watu wakumbwa na njaa Sudan Kusini:UM

Mamilioni ya watu wakumbwa na njaa Sudan Kusini:UM

Watu milioni 3.9 wanakumbwa na uhaba wa chakula nchini Sudan Kusini, hali yao ikiwa imefika hatua mbaya zaidi kwa mujibu wa vipimo vya mashirika ya Umoja wa Mataifa. Grace Kaneyia na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Grace)

Kadhalika, watu 30,000 wanaishi kwenye mazingira tatanishi na kukumbwa na hatari ya kufa kwa njaa.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Chakula na Kilimo FAO, lile la Kuhudumia Watoto UNICEF, na la Mpango wa Chakula WFP.

Mashirika hayo yametoa wito kwa pande zinazokinzana nchini humo kuruhusu usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha uweze kusambazwa bila kizuizi chochote.

Ripoti inasema kwamba idadi ya watu wanaathirika na njaa imeongezeka kwa asilimia 80 tangu mwaka jana, kutokana wa mvua, upungufu wa kazi, bei kubwa za vyakula, mafuta na mazingira magumu ya kiuchumi