Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atiwa wasiwasi kuhusu vurugu nchini Congo-Brazaville kabla ya kura ya maoni

Ban atiwa wasiwasi kuhusu vurugu nchini Congo-Brazaville kabla ya kura ya maoni

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza wasiwasi wake kuhusu vurugu iliyotokea baina ya vyama vya upinzani na serikali ya Jamhuri ya Congo, wakati ambapo kura ya maoni inatarajiwa kufanyika tarehe 25 Oktoba.

Kura hiyo ni kuhusu rasimu ya katiba mpya ambapo kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake, bwana Ban amenukuliwa akisema kwamba vurugu hizo zinatia wasiwasi sana.

Aidha amewaomba wadau wote wachague njia ya mazungumzo jumuishi ya kisiasa kabla ya kura ya jumapili, ili kutatua sintofahamu zao kwa njia ya amani.

Hatimaye ametoa wito kwa mamlaka za serikali zihakikishe haki ya watu ya kuandamana kwa amani.