Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha muungano katika rasi ya Korea

Ban akaribisha muungano katika rasi ya Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha muungano mpya wa kifamilia kati ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK na Jamhuri ya Korea ambao ulianza tarehe 20 Oktoba na kupangwa kukamilika Oktoba, tarehe 26 katika mlima Kumgang.

Katika taarifa iliyotolewa leo, Katibu Mkuu amesema anaamini hatua hizo za kibinadamu kama vile familia kuungana tena baada ya kutengana zinapaswa kuhalalishwa na kutozuiliwa kwa sababu za kisiasa na kiusalama.

Aidha Katibu Mkuu amesema anatiwa moyo na mwenendo chanya katika mawasiliano baina ya nchi hizo mbili hususan makubaliano ya mwezi Agosti, akisema anatumia utafungua njia kwa majadiliano baina ya nchi hizo, ushirikiano na maridhiano.

Hatimaye ameongeza kuwa anatarajia majadiliano haya yatachangia katika kukuza haki za binadamu, amani na utulivu katika rasi ya Korea.