Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rwanda na Somalia miongoni mwa wanachama wapya wa ECOSOC

Rwanda na Somalia miongoni mwa wanachama wapya wa ECOSOC

Rwanda na Somalia zimechaguliwa kuwa wanachama wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, pamoja na nchi zingine Tatu za Afrika ambazo ni Algeria, Nigeria, na Afrika Kusini.

Uchaguzi huo umefanyika leo katika mkutano wa Baraza Kuu ambapo theluthi moja ya nchi wanachama wa ECOSOC wamechaguliwa upya.

Kwa ujumla viti vya ECOSOC ni 54 kwa muhula wa miaka mitatu, theluthi moja ikibadilishwa kila mwaka.

Nchi zingine wanachama kutoka bara la Afrika ni Botswana, Burkina Faso, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , Ghana, Mauritania, Mauritius, Togo, Uganda na Zimbabwe.