Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za kusaka maji na usawa wa kijinsia Tanzania

Harakati za kusaka maji na usawa wa kijinsia Tanzania

Upatikanaji wa maji safi na huduma za kujisafi ambalo ni lengo namba sita la mendeleo endelevu SDGS ni miongoni mwa mahitaji muhimu katika nchi zinazoendelea. Nchini Tanzania mkoani Mara uhaba wa maji unaripotiwa katika baadhi ya maeneo na kusababisha baadhi ya wakazi kupoteza muda mwingi kusaka maji. Lakini wakati adha hiyo ikiendelea nayo, huku ukame nao ukichochea tatizo hilo, wanaume nao wamechukua jukumu la kusaidia wanawake katika kusaka rasilimali hiyo adhimu katika kuboresha utendaji kazi majumbani.

Je nini kinafanyika?Martin Nyoni wa redio washirika redio SAUT ya Mwanza Tanzania amevinjari katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo wa Mara na kutuandalia makala ifuatayo.