Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kihistoria kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Somalia waanza

Mkutano wa kihistoria kwa ajili ya kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Somalia waanza

Huko Geneva, Uswisi kunafanyika mkutano wa aina yake wa kusaidia wakimbizi wa Somalia wanaorejea nyumbani kwa hiari, mkutano unaohudhuriwa na viongozi waandamizi wa shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR, Waziri Mkuu wa Somalia, Omar Abdirashid Ali Sharmake , Waziri wa Mambo ya Ndani na Uratibu wa Serikali ya kitaifa wa Kenya, Joseph Ole Nkaissery na wengine. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Lengo na shabaha ya mkutano huo ni kujenga mazingira kwa ajili ya wakimbizi wa Somalia walioko nchi jirani ikiwemo Kenya, kurejea nyumbani kwa hiari na kuwaunganisha na jamii zaoikiwa ni pamoja na usalama na kujenga ujasiri wa wakimbizi na jamii za wenyeji ndani ya Kenya. Uchangishaji huo unalenga kukusanya dola Milioni 500 kusaidia usalama, miundombinu ya kijamii na maendeleo.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Antonio Guterres ameseme, japo hali ya Somalia imekuwa ni ngumu, lakini kuna matumaini

(SAUTI Guiteress )

“Wasomali ni miongoni mwa raia kutoka mataifa kumi ya watu wanaovuka  Bahari ya Mediterania wakielekea Ulaya mwaka 2015, lakini hata hivyo, kuna fursa muhimu , usalama, hali ya kisiasa na kiuchumi za kijamii nchini Somalia imeanza kuonyesha dalili za utulivu ”

Kwa upande wake Waziri Nkaiserry amesihi

(SAUTI Nkaiserry)

"Ni fursa kwa dunia kuchukua nafasi hii ya kusaidia kugeuza hali ya Somalia, kuimarisha juhudi za majirani zake na kusaidia katika utulivu wa jumla wa eneo."