Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya Watoto ya Zanzibar yashinda tuzo ya kimataifa

Sheria ya Watoto ya Zanzibar yashinda tuzo ya kimataifa

Sheria ya Watoto ya Zanzibar ya mwaka 2011 imeshinda tuzo ya sera za mustakabali yaani Future Policy Award.

Tuzo hiyo imetolewa mjini Geneva, Uswisi na Shirika la World future Council pamoja na Umoja wa Mabunge Duniani IPU na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.

Taarifa ya IPU imesema sheria hiyo imesaidia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu watoto na kuchangia katika kupambana na ukatili dhidi ya watoto.

Aidha kupitia sheria hiyo, serikali ya Zanzibar imeunda zaidi ya mabaraza 200 ya watoto visiwani humo ili kuwashirikisha katika uelewa na utekelezaji wa sheria.

Hamisa Mmanga Makame ni mwanasheria wa serikali.

(Sauti ya Bi Makame)