Skip to main content

Mchango wa Umoja wa Mataifa Burundi haupingiki: Mbilinyi

Mchango wa Umoja wa Mataifa Burundi haupingiki: Mbilinyi

Kulekea kilele cha maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 mwezi huu, chombo hicho kupitia mashirika yake mbalimbali kimetajwa kuwa na mchango mkubwa nchini Burundi katika maeneo mengi ikiwemo ujenzi wa amani, na hata ustawi wa jamii.

Hii ni kwa mujibu wa mwakilishi mkazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi nchini humo, UNHCR Abel Mbilinyi ambaye ameimabia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa miradi mingi imefanikiwa kutokana na Umoja wa Mataifa..

(SAUTI MBILINYI)

Hata hivyo Mbilinyi amesema kile anachotamani kukiona kinafanyika nchini Burundi..

(SAUTI MBILIYI)

Kamati maalum ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi imeundwa lakini hata hivyo haijafahamika lini maadhimisho yatafanyika.