Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaongeza juhudi za kuchunguza na kudhibiti kuenea kwa virusi vya mafua Afrika

WHO yaongeza juhudi za kuchunguza na kudhibiti kuenea kwa virusi vya mafua Afrika

Virusi vya kuambukizwa katika msimu usiotabirika pamoja na mafua ya ndege ni tishio lililojitokeza barani Afrika na hivyo kuchochea Shirika la Afya Duniani, WHO kuongoza utekelezaji wa mikakati ya kitaifa ya maandalizi dhidi ya mafua, ufuatiliaji na udhibiti kwa minajili ya kulinda raia.

Katika taarifa, WHO imesema virusi vya mafua ni hatari kivyake, lakini pia ni sababu muhimu ya ugonjwa wa kupumua kama vile Numonia , ambayo ni sababu kubwa ya kifo barani Afrika, hasa miongoni mwa watoto.

Barani Afrika, athari ya maambukizi ya mafua haijanakiliwa vizuri, ingawa taarifa ya WHO inaonyesha kwamba, virusi vya mafua vinavyozunguka katika wanyama, ikiwa ni pamoja na mafua/homa ya ndege, ni tishio kuu kwa afya ya binadamu.