Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova asikitishwa na kuenea kwa vurugu dhidi ya Maeneo matakatifu Mashariki ya Kati

Bokova asikitishwa na kuenea kwa vurugu dhidi ya Maeneo matakatifu Mashariki ya Kati

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bukova ameelezea wasiwasi wake upya kuhusu machafuko karibu na, na dhidi ya maeneo matakatifu Mashariki ya Kati, na kwa muktadha huo, ameanza mashauriano mapana ya kuhamasisha nchi wanachama wa UNESCO kuanza mjadala muafaka kwa mujibu wa mamlaka ya UNESCO .

Katika taarifa, Bukova amelaani mapendekezo yaliyowasilishwa hivi karibuni, ambayo yanayojadiliwa na Bodi Tendaji ya UNESCO, yakitaka kubadilishwa hali ya Mji Mkongwe wa Yerusalemu na kuta zake, ambao umeorodheshwa kama eneo la urithi wa dunia.

Mkurugenzi Mkuu huyo amesihi Bodi ya Utendaji ya UNESCO isifanye maamuzi ambayo yatachochea mgogoro sawia na kuhimiza heshima ya maeneo matakatifu